
Usiku wa kuamkia leo Soko Kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO, lililopo mkabala na maeneo ya Mwanjelwa jijini Mbeya linateketea kwa moto chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.


Moto huo ulianza kuwaka mnamo majira ya saa tatu usiku na kusababisha tafrani kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwepo maeneo hayo walionesha juhudi kuuzima moto huo lakini kwa bahati nzuri kikozi cha zima moto kikawa kimeishawasili na kuendelea kupambana na moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi kubwa mpaka.

Kwa upande mwingine wananchi wameonekana wakimwaga machozi na kulitupia lawama kwa Jeshi la Polisi kwa kutowaruhusiwa kusogea eneo la tukio kuokoa mali zao na kuwafyatulia risasi hewani wakati wa uokoaji.

Hii ni mara ya tatu sasa ambapo soko hili liliisha ungua mara mbili mfululizo kabla ya kuungua tena kwa mara nyingine usiku wa kuamkia leo.