REAL MADRID YAIFANYA KITU KIBAYA BARCELONA, YABEBA KOMBE LA UFUNGUZI WA MSIMU
Real Madrid imebeba Kombe la Spanish Super Cup, hiyo ni baada ya kuichapa Barcelona katika mechi zote mbili, ikiwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu imekabidhiwa kombe hilo baada ya kushinda kwa mabao 2-0.
Real Madrid ambayo inafundishwa na Zinedine Zidane ilishinda mechi ya kwanza ugenini kwa mabao 3-1, hivyo kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya Barcelona.