The House of Favourite Newspapers

SHAKA SSALI KUPAMBA KONGAMANO LA WAZALENDO SEPT. 2

0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba.

MTANGAZAJI maarufu duniani kutoka Kituo cha Redio cha Sauti ya Amerika (VoA), Shaka Ssali anatarajiwa kupamba kongamano la Meza ya Wazalendo litalofanyika Septemba 2, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, mratibu wa kongamano hilo kutoka Taasisi ya Vijana Wazalendo wa Kitanzania, Tanzania Youth Patriots (TYP), Vian Nchimbi alisema kuwa, siku hiyo kongamano litaanza rasmi saa 7 mchana hadi saa 11 jioni.

Shaka Ssali .

“Mgeni rasmi katika kongamano hili la kihistoria anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba atakayesindikizwa na watoa mada mashuhuri nchini, akiwemo Mh. Lawrence Masha, Eric Shigongo, Maria Sarungi Tsehai, Mzee Shaba na Benjamin Fernandes,” alisema Vian na kuongeza;

Eric Shigongo.

“Njooni kwa wingi ili muwe sehemu ya mjadala mpana ambapo mambo mbalimbali juu ya Utanzania wetu na dhana nzima ya uzalendo kwa jumla yatazungumzwa. Wanafunzi wa sekondari, vyuo vya elimu ya juu, taasisi mbalimbali na wananchi wote mnakaribishwa kwani kiingilio ni bure kabisa”.

Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu au ujumbe wa SMS  au WhatsApp kupitia namba 0769984781.

Kongamano hili limedhaminiwa na Clouds TV, Global TV na EF Outdoor.

MIMI NI MZALENDO, NITAHUDHURIA, WEWE JE?

Na Mwandishi Wetu

VIDEO: Serikali Yaagiza Magazeti Yote Tanzania Kusajiliwa Upya Kabla ya Oktoba 15

Leave A Reply