The House of Favourite Newspapers

TRUMP JEURI, ATOA KAULI ‘NGUMU’ KUHUSU UJENZI WA UKUTA WA MEXICO

TRUMP JEURI
Rais wa Marekani, Donald Trump.

 

Trump jeuri…

RAIS Trump amewalaumu vikali wapinzani wa chama cha Democratic kuwa wanakwamisha ujenzi wa ukuta utakaotenganisha Marekani na Mexico.

 

Amelitaka bunge la Congress kupitisha bajeti ya ujenzi wa ukuta huo ili kuzuia wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia Marekani.

 

Katika hotuba yake Trump alisema Democratic wanahatarisha usalama wa raia wa Marekani kwa kukataa hoja ya ujenzi wa ukuta.

 

Pia alisema kuwa endapo hoja yake haitaungwa mkono, yuko tayari kusimamisha shughuli zote za serikali. Hii itatokea pale mswada kuhusu ujenzi huo utakapojadiliwa bungeni Oktoba 1 mwaka huu.

 

“Wapinzani wa Democratic wanataka tusijenge ukuta. Lakini nawaambia niko tayari kufunga shughuli zote za serikali ili kujenga ukuta wa Mexico,” alisema Trump, kisha akaongeza, “Wananchi wa Marekani walinipigia kura ili nirekebishe sera za uhamiaji.”

 

Baada ya kumalizika kwa hotuba yake, polisi walikabiliana na waandamanaji ambao walipinga kauli hizo za Trump.

 

NA: DAUD MAKOBA| GPL

Comments are closed.