×

LIVE: Bomoabomoa Yahamia Sinza Legho, Kanisa, Maduka Vyasombwa

Bomoabomoa ikiendelea.

Kilio cha bomoabomoa, asubuhi hii kimehamia Sinza Legho jijini Dar es Salaam ambapo jengo ambalo zamani lilikuwa likifahamika kama 92 Club, ambalo baadaye lilibadilishwa matumizi na kuwa kanisa na maduka ya biashara mbalimbali, limebomolewa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mgogoro wa umiliki.

Hali ilivyo eneo hilo.

Bomoabomoa hiyo imeanza alfajiri ambapo wahusika wakiwa hawana taarifa juu ya kinachoendelea, walishtukia kundi la watu likianza kuvunja jengo hilo kabla ya baadaye tingatinga kuwasili na kumaliza kazi, ambapo hakuna aliyeruhusiwa kutoa kitu chochote.

Nyumba zikiwa zimeshushwa.

 

Bomoabomoa Legho wananchi hali mbaya.

 

Taharuki eneo la tukio.

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

Leave a Comment