Baada ya kuibuka taarifa za ubomoaji wa zaidi ya nyumba 17,000 Wilaya ya Kinondoni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema hana taarifa na bomoabomoa hiyo.
Makonda aliyasema hayo leo huko Kigogo na kusisitiza kwamba hata Rais Magufuli hana taarifa ya bomoabomoa hiyo na hivyo akaamuru zoezi hilo lisitishwe.
Pamoja na kumtaka Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kusimamia uamuzi huo, Makonda aliwataka wananchi waepuke kujenga na kuishi katika maeneo hatarishi na wajenge kwa kufuata taratibu zote rasmi ikiwa ni pamoja na kutunza nyaraka ili kuepuka matatizo.