×

Mwenyekiti UVCCM Aliyeshtakiwa Kujifanya Usalama wa Taifa Aachiwa

Lengai Ole Sabaya akizungumza na wanahabari baada ya kuachiwa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemwachi huru na kufuta shitaka la aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya aliyekuwa anakabiliwa na shitaka la kujifanya Mtumishi wa umma katika idara ya usalama wa taifa (TISS) baada ya upande wa Jamhuri kuiondoa shitaka ikiwa ni mara ya nne upande wa Jamhuri kuliondoa shitaka hilo ambako kwa mara tatu ililiondoa na kulirudisha tena mahakamani.

Akitoa taarifa mahakamani hapo wakili wa serikali Pernina Johakimu aliiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Nestory Barro akisema upande wa Jamuhuri imeona hajkuna haja ya kuendelea na shitaka hilo hivyo anaiomba mahakama ilifute.

Akizungumza baada ya ombi la upande wa Jamhuri Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Nestory Barro ameutaka upande wa Jamuhuri kupitia wakali huyo wa serikali kuacha tabia ya kupeleka shitaka mahakamani na kulitoa kwakuwa ni kinyume na haki za binadamu huku akimtaka wakili wa serikali kusoma vipengere vya sheria vinavyo ahinisha ukomo wa mtu binafsi au taasisi yoyote kumsumbua mtu mara kwa mara kwa kufikisha mghakama na kumwachia bila sababu za msingi.

Akizungumza nje ya Mahakama Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sambasha kwa tiketi ya CCM amesema anaishurukuru mahakama kwa kumpa haki kwakuwa yote hayo yanatokana na chuki za kisiasa huku wananchi wakieleza wanavyo athirika kwa mwakilishi wao kushitakiwa mara kwa mara.

Global TV Kenya: Cheki Polisi Walivyomnasa Jambazi Huyu

Alikiba Vs Diamond Wazidi Kuwagawa Wabunge Dodoma

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave a Comment