×

SHAKA SSALI KUONGOZA KONGAMANO LEO

SHAKA SSALI KUONGOZA KONGAMANO LEO

MTANGAZAJI wa kimataifa kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) ambaye ni mhariri wa idara hiyo na mtangazaji wa Kipindi cha Straight Talk Africa, Shaka Ssali leo (Septemba 2) anatarajiwa kuwa kati ya waongozaji katika kongamano la kihistoria la Meza ya Wazalendo litakalofanyika Ukumbi wa Nkurumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, mmoja wa waandaaji wa kongamano hilo kutoka Taasisi ya Vijana Wazalendo wa Kitanzania, Tanzania  Youth Patriots (TYP), Vian Nchimbi alisema kuwa, mbali ya uwepo wa Shaka pia watakuwepo watoa mada mashuhuri nchini akiwemo, Maria Sarungi Tsehai, Lawrence Masha, Eric Shigongo, Mzee Shaba na Benjamin Fernandes.

 

“Ratiba itaanza rasmi saa 7 mchana hadi saa 11 jioni ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba.

 

Tunawaomba wote mje kuwa sehemu ya mjadala mpana ambapo mambo mbalimbali juu ya Utanzania wetu na dhana nzima ya uzalendo kwa jumla yatazungumzwa.

 

“Wanafunzi wa sekondari, vyuo vya elimu ya juu, taasisi mbalimbali na wananchi wote mnakaribishwa kwani kiingilio ni bure kabisa,” alisema Vivian. Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu au ujumbe wa SMS au WhatsApp kupitia namba 0769 984 781. Kongamano hili limedhaminiwa na Clouds Media Group na Global Publishers.

 

MIMI NI MZALENDO, NITAHUDHURIA, WEWE JE?

 

STORI: MWANDISHI WETU| RISASI

Leave a Comment