×

FT: SIMBA 5-0 HARD ROCK, MCHEZO WA KIRAFIKI, DAR

Wachezaji wa simba wakipongezana.

FULL TIME

Dakika ya 93: Mchezo umemalizika, Simba wanapata ushindi wa mabao 5-0.

Dakika ya 92: Mchezo umepungua kasi na timu zinajiandaa kukamilisha dakika ya mwisho.

Dakika ya 91: Hard Rock wanafika langoni mwa Simba lakini mpira unaokolewa.

Dakika ya 91: Hard Rock wanafika langoni mwa Simba lakini mpira unaokolewa.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 80: Mchezo umebalansi, Simba wanacheza soka la pasi.

Dakika ya 80: Mchezo umebalansi, Simba wanacheza soka la pasi.

Dakika ya 77: Hard Rock wanapanda na kutengeneza mashambulizi lakini mipango yao inakuwa haina nguvu.

Dakika ya 72: Simba wanatengeneza mashambulizi lakini Hard Rock wanaonyesha kuwa makini.

Dakika ya 67: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

Dakika ya 72: Simba wanatengeneza mashambulizi lakini Hard Rock wanaonyesha kuwa makini.

Dakika ya 67: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

Dakika ya 61: Simba wanasogea langoni mwa Hard Rock lakini wanakuwa wameotea.

Ndemla anafunga bao la kiwango cha daraja la A, ametamba ana mpira kutoka eneo la katikati ya uwanja, akamtoka beki wa Hard Rock na kupiga shuti la mbali, likajaa wavuni.

Dakika ya 59: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!

Dakika ya 51: Gyan ameingia akiwa na kasi, anashangiliwa

Dakika ya 50: Simba wanamiliki mpira.

Simba wanapata bao zuri la tatu kupitia kwa Gyan ambaye anafunga akimalizia kazi nzuri ya Mo.

Dakika ya 48: GOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 45: Simba wamefanya mabadiliko, ametoka Luizio ameingia Nicholaus Gyan.

Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika ya 46: Hard Rock wanapata kona, inapigwa na kipa wa Simba anaudaka mpira.

Dakika ya 45: Faulo kuelekea kwa Simba, Mo anacheza vibaya katikati ya uwanja.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 40: Simba wanamiliki mpira muda mwingi.

Simba wanapata bao la pili mfungaji ni yuleyule, Mo amemalizia kazi nzuri iliyoanzia kwa Ndemla kisha Luizio.

Dakika ya 36: GOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 30: Mchezo haina kasi kubwa, Simba wametawala sehemu ya katikati ya uwanja.

Dakika ya 25: Mavugo anapata nafasi nyingine akiwa yeye na kipa anashindwa kufunga, anakaa chini akiwa haamini macho yake.

Dakika ya 23: Mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 20: Mchezo bado unaendelea kwa timu zote kupokezana kumiliki mpira.

Dakika ya 15: Simba wanaongoza bao 1-0.

Pasi nzuri kutoka kwa Said Ndemla inamfikia Mohamed Ibrahim ‘Mo’ anamchambua kipa.

Dakika ya 11: GOOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 5: Simba ndiyo wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 2: Straika wa Simba, Laudit Mavugo anakosa nafasi ya wazi akiwa yeye na lango, shuti lake linapaa juu.

Dakika ya 1: Simba wanaanza kwa kasi ndogo.

Mchezo umeanza.

Timu zote zimeishaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo.

Huu ni mchezo wa kirafiki kati ya Hard Rock ya Pemba ambao ni wageni wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru.

Leave a Comment