
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema hali ya umasikini ya katika familia yao ilimfanya ajitume zaidi kutimiza kile alichokiamini katika maisha yake.

Hayo ameyasema leo Jumamosi, Septemba 9 wakati wa Semaina ya Fursa inayoendehswa na Clouds Media Group iliyofanyika katika Ukumbi wa Naura Springs jijini Arusha.

“Ni Mungu pekee ndiye amenisaidia kufika hapa nilipo leo, Mama yangu alikuwa anachoma maandazi na sambusa wakati baba yangu alikuwa dalali.
“Lakini kwenye maisha kuna “destination” ambayo mtu anatakiwa kuchagua, nilihangaika kusoma kwa bidii. Na kumsaidia mama kuuza sambusa wakati wa mchana baada ya masomo.

“Mara ya kwanza wakati nafika Arusha nilihitaji kufanya uongozi unaoacha alama nikawafikiria bodaboda, hawa ni kundi kubwa la vijana waliojiajiri kila nilipofika walinikatisha tamaa lakini sikurudi nyuma nilifanikiwa kuwapata wahisani wakanipa pikipiki 200. Sikupenda tuzitoe bure, niliwakusanya vijana kwa makundi tukawakopesha leo hii mfuko umefikisha milioni 200.

“Vijana tufanye kazi na tuache kupigana majungu. Kikubwa fursa inafanyika mikoa yote inayopita Fiesta na lengo hasa ni kuwatia moyo vijana na kuwapa mbinu za kuweza kufanikiwa,” alisema Gambo.

Kwa upande wake, Ruge wakati akifundisha kwenye semina hiyo ambayo amekuwa akiiongoza kwa miaka mine sasa amesema;
T”ulikuwa tukihamasishana katika fursa, nadhani imetosha, tunachohitaji kwa sasa ni kufanya maamuzi.

Alitolea mfano wa zao la soya hapa nchini akisema kuwa, soya inayohitajika kwa Tanzania ni tani elfu 30, lakini inayovunwa tani elfu 5 tu ikilinagnisha na Rwanda wanaovuna tani elfu 25. Hivyo aliwataka wananchi wa Arusha kutong’ang’ania katika kilimo cha mazao ya kawaida yanayolimwa kila siku, huku akiwataka kubadilisha mitazamo ya fikra na kuongeza thamani ya mazao yao.
Katika semina hiyo ambayo kauri mbiyu yake ya mwaka huu ni FURSA ONGEZA THAMANI, Anzia Sokoni, wazungumzaji wakuu walikuwa Ruge Mutahaba, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Vijana Atony Mavunde na Hassan Ngoma.
PICHA NA HILALY DAUDI | GPL | ARUSHA