USIKU wa kuamkia leo bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ walitoa burdani ya kukata na mundu katika ukumbi maarufu wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam wakiwa wanashiriki katika tamasha maalum lililopewa jina la Full Dozi.
Twanga Pepeta waliongozwa na Luiza Mbutu, Ali Choki na Super Nyamwela ambapo walionyesha manjonjo kibao yaliyowaacha ‘hoi’ mashabiki hadi majogoo yanawika.