×

Wananchi Waomba Chakula Kifutwe Msibani

Picha si ya tukio.

BAADHI ya wananchi wa Nzengo ya Amani ‘B’ Kata ya Nyihogo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani hapa, wameuomba uongozi wao wa mtaa kuifuta ratiba ya chakula msibani ili fedha za rambirambi zinazopatika zitumike kumfariji mfiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao wa Amani, Hawa Kasonso alisema kuwa anatamani kama uongozi ungepitisha azimio la watu kuchangia rambirambi msibani pasipo kula ili pesa ambayo ingetumika kwa chakula apewe mfiwa.

“Mimi binafsi nakerwa na kitendo cha wananchi kuchangishana fedha nyingi msibani kisha fedha hizo zinaishia kununuliwa vyakula vinavyotumika katika msiba na kusahau kumtengea fungu kubwa mfiwa. Ushauri wangu tukichangia rambirambi tusile chakula ili fedha tumuachie mfiwa.

“Fedha nyingi ya rambirambi inatumika kimakosa, unakuta waombolezaji wanakule weee, halafu baada ya hapo

wanasambaa na kumuacha mfiwa hana kitu, wakati huo       atakuwa hafanyi kazi kwa siku kadhaa, sasa unategemea atakuwa anakulala nini na hapo wananzengo tunakuwa tumemsaidia nini?

“Kama mfiwa ni mwanamke basi ndiyo anateseka hasa na watoto wake, lazima tubadilieshe mfumo wa kusaidiana kwenye misibasiyo kwenda kula na kuongeza umaskini. Utadhani huwa hatuli nyumbani labda kama kuna wengine wanasubiri misiba ili wale chakula kizuri,” alisema Kasonso.

Chadema: Lissu Amevunjwa Mguu na Nyonga Lakini Jasiri, Tumuobee!

 

Akijibu hoja hiyo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyihogo, Daniel Mahela alisema kufuta suala la watu kula kwenye msiba ni sawa na kumtelekeza mfiwa kwani ukifika muda wa kula watu wanasambaa kwenda kula.

“Hoja ipo lakini kumbuka kuwa kuna watu wanafika msibani asubuhi bila kupata chochote kwenye majumba yao, sasa ukisema washinde njaa msibani na ukifika muda wa kula warudi majumbani kwao, msibani patabaki hapana watu pia itakuwa kama wamemtenga mfiwa,” alisema Mahela.

Stori: Mwandishi Wetu, Shinyanga

Leave a Comment