×

Viongozi Vyama Visivyo na Wabunge Bungeni Wamtunishia Misuli Jaji Mutungi

vyama vya siasa
Mwenyekiti wa Umoja wa Makatibu Wakuu wa Vyama Visivyo na Wabunge Bungeni, Renatus Muabhi akizungumza na waandishi wa habari.
vyama vya siasa
Mkutano ukiendelea.
vyama vya siasa
Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Taifa, Doyo Hassan akitoa ufafanuzi wa jambo.

Viongozi wa vyama vya siasa ambavyo havina wawakilishi bungeni, leo wamezungumzia namna wanavyoipinga barua waliyotumiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Prof. Francis Mutungi ya kuwataka kutoa maoni yao juu ya mapendekezo ya kubadilisha sheria ya vyama vya siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Umoja wa Makatibu Wakuu wa Vyama Visivyo na Wabunge Bungeni, Renatus Muabhi alisema:

“Msajili wa vyama alituandikia barua ya kutuomba tutoe mapendekezo yetu juu ya kubadilisha sheria ya vyama vya siasa, lakini kitu ambacho hatukubaliani nacho ni muda ambao alituandikia barua ya kutuomba tutoe mapendekezo hayo.

“Barua alituma Agosti 28, mwaka huu na alitutaka ifikapo Septemba 14, tayari tuwe tumeshatoa mapendekezo yetu juu ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa, jambo ambalo hatukubaliani nalo.

“Kama anahitaji tutoe mapendekezo yetu, tunamwomba atupatie kwanza rasimu ya sheria hiyo tuipitie kwanza ndipo tutaweza kutoa maoni ambayo yatakuwa bora katika urekebishaji wa sheria hiyo,” alisema.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment