×

NENO LA SHUKURANI KWA WAFANYAKAZI NA MKURUGENZI WETU, ERIC JAMES SHIGONGO

Maharusi, Mrisho na Catherine.

Kila jambo jema na lenye mafanikio halikosi kuwa na watu nyuma yake waliosababisha mafanikio hayo. Wakati na baada ya harusi yetu, Mrisho na Catherine, tumekuwa tukipokea pongezi nyingi kutoka kwa ndugu na marafiki, waliohudhuria na ambao hawakuhudhuria lakini wamefanikiwa kuona kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kufanikiwa kwa sherehe ya harusi yetu kulitokana na ushirikiano mzuri wa ninyi wafanyakazi wenzangu  wa idara zote chini ya mkurugenzi wetu wa Kampuni mama ya Global Publishers, Eric James Shigongo, na ndugu, jamaa na marafiki zetu.  

Aidha, kwa ushirikiano huu ambao mmeuonesha, tunaomba uendelee katika majukumu yetu mengine ya kikazi hususani katika kipindi hiki ambacho kuna changamoto nyingi za ushindani wa kibiashara. Tupambane kwelikweli ili kuleta ufanisi na hivyo kuinua kampuni yetu kwa kiwango cha hali ya juu.

Mwisho, tunakutakia mkurugenzi wetu na wafanyakazi wote wa Global Publishers afya njema, maisha marefu na baraka tele katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku.

TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI SANA.

Asanteni sana.

Mrisho & Catherine.

Leave a Comment