KAIMU KATIBU MKUU TFF ATEMBELEA GLOBAL PUBLISHERS
KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Wilfred Kidao, leo ametembelea ofisi za Global Publishers zilizoko Sinza-Mori ambako alitembelea ofisi mbalimbali za kampuni hiyo zikiwemo za gazeti la Championi na kujionea jinsi gazeti hilo linavyotayarishwa. Vilevile alifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali na wahariri wa magazeti ya kampuni hiyo akisifia utendaji kazi wao wa ufanisi.
Aliwataka wafanyakazi wa kampuni hiyo waendeleze kazi nzuri wanayofanya katika kujituma na kutoa habari za uhakika na kuvutia kwa wasomaji ili waendelee kuyasoma magazeti hayo.
(PICHA; MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS)