×

Lulu Awasili Mahakamani Kesi ya Kifo cha Kanumba – Video

Lulu akifika mahakamani.

#GlobalHabariUpdates: Muigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akiambatana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila wamewasili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mapema leo asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili ya kusababisha kifo cha Steven Charles Kanumba bila kukusudia.

Lulu ambaye kesi yake hiyo inaanza kusikilizwa tena leo, akizungumza na kitupo kimoja cha televisheni nchini, jana alisema yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena huyku akieleza kuwa taarifa za kesi hiyo alizipata kabla watu hawajaipata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.

“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa, siyo kama imeibuka tu, na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”, amesema Lulu.

Lulu aliendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.

Kesi inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena leo Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu. Lulu anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha aliyewahi kuwa muigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo April 7, 2012 .

Global Publishers itaendelea kukujuza kila kinachojiri kutoka Mahakama Kuu. Endelea kuwa karibu nasi.

====NA DENIS MTIMA | GPL===

VIDEO YA TUKIO HILO

Leave a Comment