KESI inayomkabili muigizaji wa kike, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo Jumatatu, Oktoba 23, inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa nne upande wa Jamhuri atatoa ushahidi wake.
Tayari Lulu, mama yake, Lucresa Kalugira, Mama Kanumba, Flora Mtegoa na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco, wameshafika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.
Mashahidi watatu tayari wameshatoa ushahidi wao ambao ni Seth Bosco, ACP Ester Zephania kutoka Kituo cha Polisi Oyster Bay ambaye alikwenda kumkamata Lulu na kufanya uchunguzi wa tukio hilo, na Daktari wa familia ya Kanumba, Dkt. Kagaiya.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha aliyewahi kuwa muigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo Aprili 7, 2012.