×

GLOBALTV ONLINE SASA YAJA NA TAARIFA YA HABARI SAA 12:00 JIONI LEO

IKIWA ni sehemu ya mahitaji ya watazamaji wake, kituo cha runinga cha GlobalTv Online, kuanzia leo Novemba 2, 2017, kitaanza kurusha taarifa ya habari kila siku kuanzia saa 12;00 jioni.

Taarifa hiyo ya habari itakuwa imesheheni habari zilizothibitishwa za kitaifa, kimataifa na bila kusahau sekta muhimu ya michezo na burudani. Subscribe muda huu hapa www.youtube.com/user/uwazi1

GlobalTv Online inawashukuru watazamaji wake kwa kuendelea kuwaamini na kuwaunga mkono, kwa kutazama vipindi mbalimbali vinavyorushwa na kituo hicho, pia inawaomba watazamaji hao waendelee kufuatilia vipindi vingine vipya vitakavyoanzishwa ikiwemo taarifa ya habari, ambayo inaanza rasmi leo Alhamisi.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave a Comment