×

Rammy Gallis Ageukia Ujasiriamali

Msanii wa filamu Bongo, Rammy Gallis.

SIJUI ndiyo kusema vyuma vimekaza au nikujiongeza! Msanii wa filamu Bongo, Rammy Gallis ameamua kugeukia ujasiriamali kwa sababu anahisi kwa sanaa ya Kibongo pekee haiwezi kukidhi mahitaji yake.

Gallis aliiambia Full Shangwe, kuwa ameona ajikite kwenye ndoto yake nyingine ya kufungua mgahawa wa misosi aliouita Mandoz Grill uliopo Mikocheni.

 

“Namshukuru Mungu nimetimiza ndoto yangu nyingine ya kufungua mgahawa wangu kwa ajili ya maakuli. Nimeamua nijiongeze kwa sababu vyuma vimekaza na sanaa pekee ya Kibongo, haiwezi kunifanya nikatoboa,”alisema.

Leave a Comment