Blac Chyna Ndani Ya Penzi Jipya!
MARA baada ya migogoro kuzidi na kusababisha kutemana na mzazi mwenzake ambaye pia ni kaka wa mwanamitindo, Kim Kardashian aitwaye Rob, inaelezwa kuwa mwanamitindo mwenye makeke, Blac Chyna amezama penzini na rapa, Playboi Carti.
Chyna alitumia Snapchat yake kutangaza uhusiano huo juzikati kwa kuweka video akiwa na rapa huyo wakiendesha gari mitaa ya Los Angeles.
Wawili hao walionekana pia wakiwa pamoja kwenye jengo la ComplexCon huko Long Beach, California.
Uhusiano huo umekuja wakati ambao Chyna naye ameingia kwenye muziki wa kurap.