The House of Favourite Newspapers

Okwi, Juuko Wawazimia Simu Viongozi

0

 

Wachezaji wa Simba wakipongezana.

WAGANDA, Emmanuel Okwi na Juuko Mur­shid, wameanza vituko ndani ya timu hiyo baada ya kwenda kwao na kuchelewa kurudi kujiunga na wenzao wanaojiandaa na mch­ezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons.

 

Simba ambayo ipo jijini Mbeya, itawakosa nyota hao katika mchezo wao wa kesho Jumamosi ambapo Okwi ni majeruhi, huku Ju­uko akiwa ni mzima, lakini hajaungana na wenzake.

 

Wawili hao waliondoka wiki mbili zilizopita kwenda kujiunga na timu yao ya taifa iliyokuwa inajiandaa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Congo Brazzaville.

 

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya kambi ya timu hiyo iliyopo Mbeya, zi­nasema kwamba, wachezaji hao haijulikani lini watare­jea huku simu zao zikiwa hazipatikani.

 

“Bado Okwi na Juuko hawajarudi kambini tangu walipoenda kwao kujiunga na timu ya taifa, na mpaka sasa simu zao hazipatikani hivyo taarifa zao za lini watarejea hazi­fahamiki,” alisema mtu huyo.

Alipotafutwa mratibu wa timu hiyo, Abass Ally, alisema: “Juuko na Okwi kweli hawa­jafika na sina taarifa zao, hivyo siwezi kusema lolote.”

Stori: Musa Mateja | Global Publishers

Leave A Reply