
PREZDAA wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Patcho Mwamba amesema anamuhurumia msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuhukumiwa miaka miwili jela kwa kusema kuwa; “Jela siyo kuzuri”.
Lulu amefungwa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba, tukio hilo lilitokea Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican jijini Dar.

Patcho amesema anamuhurumia msanii huyo japo kwa upande mwingine ashukuru kutokana na udogo wa miaka aliyofungwa ikiwa ni tofauti na hukumu nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa kutokana na kesi za mauaji.

“Kiukweli jela siyo kuzuri na mimi namuonea huruma sana Lulu, lakini niseme ashukuru kwa namna moja kwani hukumu ambayo amepewa ni ndogo sana ukilinganisha na aina ya kesi hiyo ya mauaji ambapo tumeshuhudia hukumu zikiwa kubwa,” alisema Patcho.