





Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema ni makosa kisheria kwa mtu yeyote kutoa takwimu zisizo rasmi na badala yake, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka kisheria ya kutoa rasmi takwimu.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika ambayo kitaifa yamefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Posta jijini Dar es Salaam, Chuwa amesema takwimu zinazotolewa na ofisi yake, hukusanywa kitaalamu na huwa na vigezo vya kimataifa vinavyoweza kutumiwa na serikali kwa ajili ya mipango mbalimbali ya maendeleo ya wananchi wake.
DENIS MTIMA/GPL