×

Ben Pol Amtambulisha Ebitoke Fiesta

Ben Pol akitumbuiza stejini katika Tamasha la Fiesta 2017 Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Ebeitoke akiingia stejini.
…Akimwelezea hisia zake Ben Pol.
Wakiimba kwa kujibishana.
Ebitoke akiwa amekaa akiimba wimbo wa Ben Pol wa Moyo Mashine.

Mchekeshaji maarufu kupitia mitandao ya kijamii, Ebitoke, jana aliibuka stejini kumfuata Ben Pol ambaye awali alionyesha hisia za kumtaka kimapenzi.  Alipopanda stejini, alimweleza Ben Pol kwamba alikuwa anampenda na ataendelea kumpenda na aliwataka Watanzania wamwelewe hivyo, jambo ambalo lilizua shangwe kutoka kwa mashabiki.

(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

Leave a Comment