
KAMPUNI ya kubashiri Tanzania SportPesa imewakabidi vifaa vya michezo wabunge wa Bunge la Tanzania kwa ajili ya michuano ya mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki inatakayoanza kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa SportPesa, Tarimba Abass, amesema kwamba wametoa vifaa hivyo kwa wabunge ili viweze kuwapa hamasa kwenye michuano hiyo mikubwa hapa Afrika Mashariki.

“Nia yetu ni kuwasaidia wabunge wetu ili wawe na hamasa ya kucheza na kuhakikisha wanaibuka mabingwa wa michuano hiyo, maana vifaa tulivyotoa vimejumuisha michezo yote watakayoshiriki kuanzia kesho.
“Utaona tumetoa jezi za mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu na mingine mingi,” alisema Tarimba.
(PICHA, HABARI: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS)