The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Babu Seya na Papii Kocha Waachiwa Huru

Wanamuziki Nguza Viking’ Babu Seya’ (kulia) na mwanawe Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wakiwa nje ya Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam leo baada

Wanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe Johnson Nguza (Papii Kocha) wametoka jioni hii katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kulakiwa na familia na mashabiki wao.
Taarifa zaidi baadaye.

Wananchi wakiwa nje ya gari lilotumika kuwabeba wasanii hao.

Mapema leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, alitangaza msamaha kwa  wafungwa wakiwemo Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza (Papii Kocha) ambao walifungwa jela maisha mwaka 203 katika Gereza la Ukonga ambap rais aliagiza waachiwe huru mara moja kutoka gerezani.

 

Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.

 

Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru Mbangu na Chichi Februari 2010.

PICHA; RICHARD BUKOS, GPL

VIDEO: JPM Amsamehe Babu Seya na Familia Yake, Sasa Wapo Huru

 

Comments are closed.