SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuthamini wajasiriamali wa viwanda vya kutengeneza nguo hapa nchini vinavyoendelea kukua na kukidhi mahitaji ya wanachi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, wakati wa sherehe ya kutimiza miaka 25 ya taasisi ya TGT iliyofanyika katika Viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta jijini Dar es Salaam.
Taasisi hiyo inayojishughulisha na masuala ya wajasiriamali, pi imebadilisha jina la mwanzo kutoka Tanzania Gatsbay Trust na kuwa Tanzania Growth Trust.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Growth Trust, Oliver Lwena amesema kuwa lengo la taasisi yake ni kuendelea kufundisha wajasiriamali wadogo kwa wakubwa ili kutengeneza ufanisi wa kujikwamua kiuchumi na maemdeleo na hasa elimu ya juu ya masuala ya kibiashara.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments are closed.