×

Pialali, Shiva Wapima Uzito Kuzichapa Kesho Bagamoyo

Mabondia wakipima uzito.

MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Mtanzania, Idd Pialali na Shiva Gurgaon mapema leo wamepima uzito tayari kwa pambano la ubingwa wa kimataifa litakalopigwa kesho Bagamoyo mkoani Pwani

 

Shiva akipima uzito.

Katika pambano hilo ambalo linatarajia kufanyika kwenye Ukumbi wa Travel Lodge ambapo litarushwa live na Global Tv Online.

Mabondia hao wametambiana kwa kila moja kuibuka bingwa wa mkandao huo wa UBO kutokana na maandalizi makali walioweza kuyafanya.

Mabondia wakipima uzito.

Shiva alisema: ” Kikubwa hapa kilichonileta ni kuondoka na huu ubingwa wa hili pambano hakuna kitu kingine, simjui mpinzani wangu lakini hatoweza kutoka salama katika mikono yangu.”

Kwa upande wa Pialali amendelea kusisitiza kuwa bondia huyo hatoweza kumaliza raundi tano kutokana na kufanya maandalizi ya uhakika.

Picha Stori: Ibrahim Mussa, Bagamoyo, Pwani.

 

Gazeti Jipya la Michezo, ‘Spoti Xtra’ Lazinduliwa Dar, Mtaani Kila Jumapili