
GAZETI jipya la Michezo na Burudani la Spoti Xtra, limezinduliwa rasmi Ijumaa wiki hii, jijini Dar es Salaam. Spoti Xtra limeanza kutoka leo Jumapili na litakuwa mitaani kila Jumapili kwa Shilingi 500 tu huku likiwa limesheheni matukio na chambuzi zilizofanyiwa kazi na waandishi na wahariri waliobobea.