×

Swansea Wamfukuza Kocha, Wanamtaka Van Gaal

Kocha wa zamani wa Man­chester United, Louis van Gaal.

FUKUZAFUKUZA mako­cha katika Premier League im­eendelea kushika kasi ambapo Klabu ya Swansea City imemfukuza kazi Paul Clement kutokana na ma­tokeo mabaya ya timu hiyo.

 

Mara baada ya kutoka kwa tangazo hilo, tayari kocha wa zamani wa Man­chester United, Louis van Gaal anatajwa kuwaniwa na timu hiyo huku majina ya makocha wengine yanayotajwa kupewa nafasi pia ni bosi wa zamani wa West Ham, Slaven Bilic na Ronald Koeman ali­yekuwa akiinoa Everton.

 

Swansea kwa sasa ndiyo inayoshika mkia katika Premier ikiwa im­eshinda michezo mi­tatu tu kati ya 18 ya msimu huu.

 

Pamoja na tetesi hizo, mapema wiki hii, Van Gaal, 66, alinukuliwa akise­ma kuwa bado anaamini atare­jea katika soka kwa kuwa kuna kazi hakuimal­iza baada ya kufukuzwa Man United mwaka 2016.