×

MWENYEKITI UVCCM TAIFA, JOKATE WATEMBELEA OFISI ZA GLOBAL

Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) akiongea na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James alipomtembelea ofisini kwake leo. Kushoto ni Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Jokate Mwegelo.

MWENYEKITI wa taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James,  leo ametembelea ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo.

 

Kheri James akisalimiana na mfanyakazi wa kitengo cha usambazaji cha Global Publishers, Nasra Mressa.

Mwenyekiti alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na  Chipukizi  wa UVCCM, Jokate Mwegelo.

 

…Akitambulishwa kwa wafanyakazi wa Idara ya Tehama (IT) na mkuu wa kitengo cha Global TV Online, James Range (wa pili kulia).

Akiwa ofisini hapo, alisema amefurahi kujionea kazi zinazofanywa ambapo  alifarijika kuona kampuni hiyo ikiwa na vijana wengi wakifanya kazi hapo ambao ndiyo nguvu ya taifa la kesho.

Jokate akimtambulisha Kheri James na viongozi aliofuatana nao kwa Mhariri Mtendaji wa Global Pubshers Ltd, Saleh Ally (kushoto).

 

Kheri James na Salehe Ally wakisalimiana.

 

Salehe Ally akizungumza jambo.

 

Mkuu wa Idara ya Tehema, Edwin Lindege, akisalimiana na Kheri James.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

KUTAZAMA MAHOJIANO YA KHERI ALIYOFANYA NA GLOBAL TV ONLINE ALIPOTEMBELEA OFISI HIZO, ENDELEA KUTEMBELEA YOU TUBE CHANNEL YA GLOBAL TV ONLINE