×

Mwili wa Mary Bukos Waagwa Dar

Waombolezaji wakibeba mwili wamarehemu.

WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na Meneja Mkuu wao Mkuu, Abdallah Mrisho leo Desemba 30, 2017 wameungana na ndugu jamaa na marafiki kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa mdogo wa Mwandishi na Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni hiyo, Richard Bukos, marehemu Merry Bukos.

 

Richard Bukos (wa pili kulia) akiaga mwili wa dada yake, Mary Bukos.

Mwili wa marehemu Mary aliyefariki dunia Desemba 28 mwaka huu baada ya kuugua ghafla, umeagwa nyumbani kwao Mburahati jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika Makaburi ya Makulumra.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) akiaga mwili wa marehemu.

Ndugu, jamaa na marafiki wamejitokeza katika kumsindikiza katika nyumba yake ya milele ambapo mwili wa marehemu umezikwa jioni hii katika makaburi hayo.

 

Mrisho akimpa pole Richard Bukos.

 

Mhariri Mwandamizi wa Global Publishers, Elvan Stambuli akimpa pole Bukos.

 

Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.

 

Ni hudhuni na majonzi.

 

 

NA DENIS MTIMA | GPL