×

Global Publishers App Yatikisa Mitandaoni, Wajanja Wamiminika Kujiunga

Washindi wakiperuzi Global TV kupitia Global Publishers App kwenye jukwaa la burudani la Dar Live usiku wa kuamkia leo.

 

APPLICATION mpya ya Global Publishers inayopatika kwenye mfumo wa Android na iOS imezidi kutikisa mitandaoni huku maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakimiminika kujiunga na App hiyo ya kijanja ambayo inaongoza nchini kwa habari na matukio ya papo kwa hapo.

 

Katika shangwe za mkesha wa mwaka mpya zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ambapo palikuwa na shoo ya kibabe iliyogongwa na Stamina, Young Killer, Jay Moe, Q-Boy, Coyo na wengine, mashabiki na wadau wengine waliokuwepo ukumbini hapo walimiminika kujiunga na Global Publishers App ambayo ilikuwa ikirusha LIVE shoo hiyo kupitia Global TV Online ambayo inapatikana ndani ya App hiyo.

 

 

Baada ya kupakua na ku-install Global Publishers App, mashabiki walijiunga na Global TV Online kwa ku-subscribe ambapo washindi wote walizawadiwa T-Shirt mpya za Global Publishers App.

 

Ndani ya Application hiyo kuna habari za matukio mbalimbali ya kijamii ndani na nje ya nchi, matukio ya papo kwa hapo, YouTube channel ya Global TV Online, simulizi, hadithi na vitabu vya mtunzi mahiri, Eric Shigongo, magazeti yote ya Global Publishers, nyimbo zote mpya za Bongo Fleva na za mamtoni.

 

Global Publishers App inapatikana hapa.