×

Simanzi, Majonzi na Vilio Kuagwa kwa Mwanahabari Justine Limonga

Waombolezaji wakisubiri kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu kwenda eneo maalumu ilipo kufanyika ibada hiyo.

NI SIMANZI, majonzi na vilio vimeikumba tasnia ya habari kufuatia kumpoteza mwanahabari mwenzao, Justine Limonga ambaye mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

Waombolezaji na wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari wa Uhuru FM, Justine Limonga, wakati ukiwasili Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa kabla ya kufanyika mazishi yake Makaburi ya Saku yaliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.

 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mwanahabari, Justine Limonga.

Katika tukio hilo, Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, ameongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki katika ibada ya kuaga mwili wa mwanahabari huyo.

 

Familia ya marehemu ikiwa kwenye ibada hiyo.

 

Akizungumza katika ibada hiyo, Polepole alisema CCM na tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa bado akitegemewa. “Tumempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akitegemewa kama chama tutaangalia namna ya kuisaidia familia yake,” alisema Polepole.

 

Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, ikitoa burudani.

Akizungumzia msiba huo, Mkurugenzi wa Nduvini Auto Garage, Alhaji Ahmed Msangi alifafanua Limonga enzi za uhai wake na kuahidi katika kipindi hiki cha kufunguliwa kwa shule, kmpuni yake itawanunulia vifaa vya shule, sare na kuwalipia karo wakati wakisubiri kukaa na familia kuona namna ya kuwazesha kielimu watoto wa marehemu.

 

Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, Philo Mbunda, akitoa mahubiri.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali alisema kifo cha mwanahabari huyo aliyekuwa mwajiriwa wao kimeacha pengo kubwa ambalo halitazibika.

Wombolezaji katika ibada.

 

Alisema Limonga alikuwa mhariri na mbunifu na aliweza kuongoza vipindi mbalimbali ambavyo vilipendwa na wasikilizaji wa Uhuru FM ambapo aliahidi stahiki zote za marehemu kama mwajiriwa zitapatikana kwa wakati.

 

Ibada ikiendelea.

 

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, dini, siasa wanamuziki na wanahabari na wananchi iligubikwa na majonzi na baadhi ya watu kushindwa kujizuia kulia.

 Mwanamuziki Nguri, John Kitime akizungumzia jinsi alivyomfahamu marehemu Limonga.

 

Akitoa mahubiri kwenye ibada hiyo Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani,  Philo Mbunda alisema mwenzetu Limonga amemaliza kazi ya hapa duniani je sisi tuliobakia tumejiandaeje?

 

Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Moni Nyangasa, akizungumza kwenye ibada hiyo.

 

Mbunda alisema kila mtu anapaswa kujitafakari maisha yake ya kiroho kabla ya kifo na hivyo ndivyo Mungu wetu anavyohitaji.

 

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, akizungumza kwenye ibada hiyo.

Limonga alifariki dunia Desemba 30, mwaka jana katika Hospitali ya TMJ alikolazwa akitibiwa na ameacha mjane na watoto wawili ambapo mazishi yake yamefanyika leo katika Makaburi ya Saku yaliyopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mbunge wa zamani wa Temeke, Abbas Mtemvu akimzungumzia marehemu Limonga.

 

Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu, akizungumza.

 

Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akizungumza katika ibada hiyo.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akiwapa pole wafiwa.

 

Mwanamuziki nguri, Hussein Jumbe, akiimba wimbo maalumu aliomtungia mwanahabari Justine Limonga.