×

Mwandishi wa Championi Ajitwisha Jiko

Mwandishi wa gazeti la Championi linalotolewa na Global Publishers, Sweetbert Lukonge akimvalisha pete mke wake, Amina Hussein, katika harusi iliyofanyika katika ukumbi wa Kuala Lumpur, Sengerema, Mwanza, hivi karibuni.
…Akifungishwa ndoa na mashehe.
…Sweebert akimwekea mkono mkewe.
Wanandoa hao wakiwa katika pozi la kufurahia harusi yao.

MWANDISHI wa gazeti la Championi linalotolewa na Global Publishers, Sweetbert Lukonge,  hivi majuzi aliuacha ukapera baada ya kufunga ndoa na Amina Hussein huko Sengerema, Mwanza, ambapo baadaye palifanyika sherehe ya ‘kufa mtu’ katika ukumbi wa Kuala Lumpur mjini Sengerema.

Uongozi na wafanyakazi wa Global Group wanawatakia maharusi hao kila la heri katika maisha ambayo wameyaanza wakiwa pamoja.