The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yatoa Pole Kwa Familia Ya Athuman Hamis

Kampuni ya Vodacom Tanzania inatuma salamu za pole kwa familia ya  aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali ya Daily News  na Habari Leo, Athumani Hamis Msengi, aliyefariki  jana  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 

Vodacom Tanzania PLC pamoja na taasisi yake ya kuhudumia jamii ya Vodacom Tanzania Foundation imepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Athumani Hamis na inatoa pole kwa familia, mwajiri na wadau wote wa tasnia ya habari.

Aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamis Msengi enzi za uhai wake.

“Kifo chake cha ghafla kimetuhuzunisha sana ikizingatiwa kuwa  marehemu alikuwa  akishirikiana nasi wakati wote kwa karibu  katika kipindi chote ambacho alikuwa bado hajapata ajali na baada ya kupata ajali tumekuwa naye karibu”

 

Daima tutaendelea kumkumbuka  marehemu Athuman Hamis na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na tupo pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

 

Imetolewa na  kitengo cha Uhusiano

Vodacom Tanzania PLC

Comments are closed.