
SIMANZI na majonzi vimetawala wakati wa misa ya kumuombea marehemu Anastazia Mayunga ambaye ni Mama wa Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa CHADEMA, Wakili Peter Kibatala,katika Parokia ya SUA, Mjini Morogoro leo Januari 13, 2017.

Viongozi mbalimbali wa Chadema, ndugu jamaa na marafiki wameungana na Kibatala katika kumuaga mama yake aliyefariki dunia juzi Alhamisi, Januari 11.

Baadhi ya viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika (Mb), Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick Ole Sosopi, Godbless Lema, Susan Kiwanga, Meya Isaya Mwita na wengine.

Aidha, chama hicho kimeahirisha mkutano wake wa Kamati Kuu ya Chama uliokuwa ufanyike leo jijini Dar es Salaam ili kupisha shughuli ya kuaga mwili wa Mama Kibatala, hivyo mkutano huo utafanyika siku nyingine.


PICHA NA CHADEMA MEDIA.