The House of Favourite Newspapers

SIMANZI! Mtoto Miaka 11 Ajiua Baada ya Kukataliwa Ombi Lake – Video

MTOTO mmoja mwenye umri wa miaka 11 ameamua kujiua kwa kujinyonga baada ya ombi lake la kuhamishwa shule kukataliwa huko nchini Kenya.

 

Taarifa zinasema kuwa mtoto huyo kutoka kijiji cha Ongata Rongai amechukua uamuzi huo mgumu baada ya mama yake kumuambia hana uwezo wa kumpeleka shule binafsi anayotaka, na kumtoa kwenye shule ya umma aliyokuwa akisoma.

 

Baada ya mama yake kutoka kwenda dukani moto huyo ambaye ni wa kwanza kuzaliwa kwenye familia ya watoto watatu, alichukua kamba na kujinynga sebuleni kwao, na mama mtu kukuta mwili wa mtoto wake ukining’inia.

 

Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo hakukuwa na ugomvi wowote baina yao zaidi ya kushindwa kutekeleza ombi lake, na jeshi la polisi kuanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo, kwani wanashindwa kuelewa kwa nini mtoto huyo hakwenda shule na kuamua kubaki nyumbani,  wakati shule zimeshafunguliwa.

Comments are closed.