×

Kumbe Linah Wala Hashtuki Mwenzenu

Linah Sanga a.k.a Ndege Mnana.

BINTI mwenye sauti nyororo, Linah Sanga a.k.a Ndege Mnana amefunguka kuwa haumizwi na wanamuziki wa kike wanaotamba hivi sasa.

Akizungumza na Spoti Extra,Lina alisema kuwa watu wengi wanadhani atatetereka na vipaji vilivyoibuka lakini wala hata haiko hivyo kwani anajua nini cha kufanya na kwa wakati gani.

Msanii huyo anaamini kuwa kila mwanamuziki ana mashabiki wake hivyo haumizwi kichwa zaidi anafurahi muziki unakuja kwa kasi ya aina yake na utakuwa na mvuto zaidi tofauti na siku za nyuma.

“Watu wengi wananiuliza nimejipanga vipi kukabiliana na wanamuziki wapya wanaofanya vizuri wakati mimi siumizwi kichwa na wao kwangu ni kutoa kitu kizuri na kuwapa mashabiki wangu ladha walioizoea,”alisema Linah ambaye alijifungua mtoto wa kike mwaka.

Tamko la JPM Lamtesa Linah