×

Mfaransa wa Simba Aanza Kazi Rasmi, Shuhudia Mziki Wake

Kocha Pierre Lechantre akifanya yake uwanjani.

Kocha Pierre Lechantre raia wa Ufaransa, ameanza kazi yake ya kuiona Simba SC ambayo sasa iko kileleni mwa Ligi Kuu  Tanzania Bara akichukua mikoba ya Mkameruni, Joseph Omog.

 

Msaidizi wake akiwa uwanjani hapo.

Mazoezi ya Simba jioni hii yanafanyika kwenye Uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.

Lechentre anasaidiwa na makocha wengine wawili ambao ni Masoud Djuma raia wa Burundi pamoja na Mohamed Habibi kutoka Tunisia ambaye amejiunga na Simba akiwa pamoja na Lechantre.

NA MUSA MATEJA | GPL