VIKAO vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo vimeanza rasmi mjini Dodoma ambapo wabunge wapya watatu, leo wabunge wapya watatu wa CCM kula kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.Walioapishwa ni Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Justin Monko (Singida Kaskazini) na Dk Stephen Kisurwa wa Longido.
Pia, Dk Tulia aliomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama ambaye alifariki dunia Novemba mwaka jana.