×

WASANII WAZUA TAHARUKI STENDI

BAADHI ya wasanii wa filamu za Kibongo, mapema leo wamezua taharuki na kugeuka kivutio kwa abiria katika stendi ya daladala ya Sinza (Mawasiliano) baada ya kuonekana wakirekodi filamu katika muonekano wa maisha ya madereva na makondakta wa daladala.

Baadhi ya wasanii walioshangaza wengi kwa kuvaa uhalisia wa kazi hiyo kwenye filamu ya Kashinde, ni pamoja na Luckiness Mokiwa na Halima Yahya ‘Davina’ kitendo kilichosababisha baadhi ya watu kuacha majukumu yao kwa muda na kubaki wakiwashangaa.

 

 

 

Hapa chini ni picha chache za tukio hilo: 

Habari/Picha: Brighton Masalu