





MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kumtia mbaroni kiongozi wa dini (mchungaji) anayedaiwa kuzaa watoto wawili na mwanafunzi aitwaye Selina, kisha kumtelekeza.
Makonda ameyasema hayo leo Februari. 10, 2018 wakati akitatua kero za wananchi wa Dar es Salaam alipokuwa akifanya mkutano nao katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo ameagiza mchungaji huyo akamatwe kabla ya kesho Jumapili.
Vilevile Makonda amesimamisha shughuli zote za mabaraza ya kata kwa wilaya zote za mkoa wake pamoja na kesi zote zilizokuwa zikiendeshwa na mabaraza hayo hadi utaratibu wa kupitia upya taaluma za wanasheria wa mabaraza hayo utakapofanyika.
Aidha Makonda amewataka makatibu tarafa kuanza kutembelea mabaraza hayo kuanzia Jumatatu ijayo ili kuziainisha kesi hizo na kuanza kuzitatua.
NA DENIS MTIMA/GPL