WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo, Februari 14, 2017 amezindua Jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Amana, iliyopo Ilala jijini Dar, ambalo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.2, jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia wanawake 100 wanaojifungua.
Katika hafla hiyo, Majaliwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa namna anavyo anapambana kutafuta wadau kusaidia kujenga miradi ya maendeleo nchini.