×

Mwili wa Daniel John Anayedaiwa Kuuawa Waagwa Dar

Ibada ya kumuombea mareemu ikiendelea kanisani.

 

MWILI wa aliyekuwa Katibu wa Chadema Kata ya Hananasif, Daniel John umeagwa nyumbani kwake na kufanyiwa ibada katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Anna, Hananasif, leo Jumanne, Februari 20, 2018, kabla ya kusafirishwa kuelekea Iringa kwa maziko.

 

Mwili ukiingizwa kanisani.

 

Daniel John anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

 

Katibu wa BAVICHA Taifa, Julius Mwita, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, aliyeagwa leo na kusafirishwa kuelekea Iringa kwa ajili ya maziko, ibada imefanyika Parokia ya Mt. Anna, Hananasif.

 

Makamu M/kiti wa CHADEMA Bara, Prof. Abdallah Safari,akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, aliyeagwa leo na kusafirishwa kuelekea Iringa kwa ajili ya maziko, ibada imefanyika Parokia ya Mt. Anna, Hananasif.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe, Amina.