×

Live Updates Kutoka Muhimbili: Kuagwa kwa Mwili wa Akwilina

Jeneza lenye mwili wa marehemu likipandishwa kwenye gari.

NDUGU, jamaa, marafiki na Watanzania wengine wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuuchukua mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini ambaye ataagwa leo katika viwanja vya chuo hicho.

Jeneza lenye mwili wa marehemu likipandishwa kwenye gari.

 

Taswira halisi inaonyesha ndugu wakifanya maandalizi ya kuchukua mwili wa Akwilina na kabla ya kuupeleka NIT ambako utaagwa na baadaye nyumbani kwao Mbezi kisha kusafirishwa kwenda Rombo kuzikwa.

 

Ndugu wakiwa eneo l chumba cha kuhifadhia maiti, Muhimbili.
Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

LIVE: MWILI WA ‘AKWILINA’ UKICHUKULIWA MUHIMBILI (VIDEO)