×

FT: NDANDA 1-2 YANGA KUTOKA NANGWANDA

MPIRA UMEKWISHAAAA

DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
Dk 90, Yanga wanapeleka shambulizi ndani ya lango la Ndanda, lakini Ngassa anaokoa

Dk 88, kona inachongwa na Mwashiuya lakini mwamuzi anasema ni faulo
Dk 88, Mhilu anaingia vizuri kabisa hapa, mpira wake wa krosi unaondolewa na kuwa kona ya Yanga
DK 86 Martin anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Yusuf Mhilu upande wa Yanga

KADI Dk 85 Ahmed Msumi wa Ndanda analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Yondani

KADI Dk 80, Mwashiuya analambwa kadi ya njano baada ya kuurusha mpira nje kwa jazba
Dk 78, Ngassa anawachambua Yanga na Yondani analazimika kumuweka chini hapa lakini anasalimika kadiSUB Dk 77 Ally Selemani anaingia upande wa Ndanda kuchukua nafasi ya TibaDk 76 John George anatandika mkwaju matata kabisa wa adhabu lakini kidogo unapita juu ya mtambaa wa panya wa lango la Yanga, goal kick

Dk 73, Kessy anaingia vizuri kabisa upande wa mashariki lakini anawekwa chini na mwamuzi anasema faulo ipikwe kwenda Ndanda
Dk 72, kona inachongwa na Mwashiuya lakini Ndanda wanaondosha hapa
Dk 71, Ndanda wanalazimika kufanya kazi ya ziada, wanaokoa na kuwa konaaaa
Dk 70 mchezaji mmoja wa Ndanda yuko chini, inaonekana amelala mwenye inawezekana ni maumivu ya misuli
Dk 69 Yanga wanachofanya wanapeleka mashambulizi mengi ya juujuu

DK 50 Raphael Daud yuko chini pale akimlalamikia mwamuzi namna alivyoangushwa. Anatolewa nje kwenda kutibiwa
GOOOOOOOOO Dk 46, Kapama anaukwamisha mpira wavuni akiunganisha pasi safi kabisa ya Ngassa
Dk 45 Mechi inaanza kwa kasi Ndanda wakionekana wanataka bao la mapema ili kuwapa Yanga presha

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZADk 45, Abdallah naye anaachia mkwaju lakini hakulenga lango
Dk 44, Majogoro naye anaachia mkwaju hapa lakini hakulenga lango
Dk 42, krosi nzuri ndani ya lango la Ndanda, Kisubi anatokea na kudaka vizuri kabisa hapa

SUB Dk 40 Waziri Majogoro anaingia kuchukua nafasi ta Baraka upande wa Ndanda
Dk 40, anakwenda kupiga Tshishimbi, kipa anadaka na kuuficha kabisa

PENAAAAAAAAAAAAAAT Dk 36, Yanga wanapata penalti baada ya beki wa Zabron kuunawa
Dk 34, Yanga wanachofanya ni kuupoza mpira wakisikilizia mabao yao mawili lakini wanashambulia kwa kushtukiza kila wanapopata nafasi
Dk 32, Martib anaingia vizuri lakini anaanguka na kipa anauwahi mpira
GOOOOOOOOO Dk 29 Kessy anachambua kama karanga kabla ya kuandika bao saaaafi la pili
DK 28, pasi ya Buswita, Martin anajaribu lakini ni shuti mtoto
Dk 25 Yanga wanalazimika kumuweka chini Ngassa, lakini mpira faulo naye anapiga nyanya kabisa na Rostand kama maji anadaka
Dk 23 nafasi nzuri nyingine kwa Yanga, kipa anaugusa, Ndanda wanaokoa
Dk 20, kona maridadi ndani ya lango la Ndanda, kipa Kisubi, anatoka na kuupiga ngumi
Dk  20, Ajibu anaachia mkwaju matata kabisa lakini kipa anaokoa kwa umaridadi kabisa. Kona
Dk 19, Ndanda wanapata kona, inachongwa lakini Yondani anaruka na kuokoa
Dk 19, inachongwa faulo vizuri na Ajibu, inaokolewa vizuri
Dk 18, Yanga inapata adhabu nje kidogo ya eneo la Ndanda
DK 15, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini mpira wa shuti la tik taka, unaishia mikononi mwa Rostande
Dk 13, inaonekana kuna makosa mengi sana katika difensi ya Ndanda na wanapaswa kuwa makini

Dk 10 shuti kali katika lango la Yanga, safari hii kipa yuko makini anaokoa, unamtoka anadaka tena
Dk 8, kona nyingi ya Ndanda, lakini Yanga wako makini wanaokoa hapa
Dk 7, Ndanda wanapata kona, inachongwa hapa, Rostand anaokoa na kuwa kona tena
GOOOOOOOO Dk 6, Buswita anafunga kwa ulaiiiini baada ya uzembe wa kipa na mabeki.
Dk 4, Ngassa tena anaingia vizuri, anapiga shuti la chinichini, goal kick
Dk 3, Ngassa anaachia mkwaju mkali, nusura afunge lakini hakuwa makini

 

Dk 1 Ndanda FC ndiyo wanaanza kushambulia kwa kasi