
MBUNGE wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Moses Nnauye amesema atawashtaki bungeni wakandarasi wanaotekeleza mradi wa maji jimboni kwake kwa uzembe wanaoufanya wa kuchelewesha kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa.
Nape amesema hayo juzi Alhamisi jimboni kwake Mtama ambako amekwenda kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ukiwemo mradi huo wa maji utakaonufaisha vijiji sita.
“Mlisema tatizo ni pesa, nimepambana mpaka pesa imepatikana, mkasema tatizo ni pampu, mnainunua mwezi mzima? Sasa niwaambie ‘nitawapig’ bungeni kwa sababu naona mnanichezea. Mradi huu usipokamilika wananchi wangu hawawezi kunielewa,” alilalama Nape.