×

VODACOM YAZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE

Mmoja wa wanawake aliyetunukiwa cheti kutoka Vodacom, Happynes Shuma (kulia) kutokana na mchango wake wa kuhamasisha, kujitambua kwa wanawake na kutoa mchango  chanya wa kuleta mabadiliko katika jamii ya wanawake.

…Akishikilia cheti alichotunukiwa katika hafla hiyo.

Mkuu wa Maduka ya rejareja kotoka Vodacom, Prigita Steven (kushoto)  akikabidhiwa cheti kutokana na mchango wake kwa jamii.

Taswira ilivyoonekana katika hafla hiyo.
...Happynes akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

Hafla hiyo ikiendelea. 

MTANDAO wa simu za mkononi wa Vodacom Tanzania, leo umezindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa hafla fupi iliyofanyika  makao makuu ya mtandao huo yaliyopo Victoria  jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali wa mtandao huo.

 

Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kumwezesha mwanamke  kujikwamua na kutumia fursa zilizopo kufikia malengo yake kimaendeleo.

 

Pia mtandao huo umewatambua na kuwatunuku vyeti mabingwa wawili wanawake wanaohamasisha kujitambua kwa wanawake na kutoa mchango  chanya wa kuleta mabadiliko katika jamii ya wanawake.