The House of Favourite Newspapers

Mafufu Amwanika Mrithi wa Mkewe!

DAR ES SALAAM: Baada ya miezi kadhaa kupita tangu aamue kuokoka na kuachana na mambo ya kidunia hali iliyosababisha mkewe Salma Sadiki kumkimbia kwa kuwa walikuwa wamefunga ndoa ya Kiislamu, hatimaye staa wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu amemwanika mrithi wa mama watoto wake huyo.

 

Picha za mrembo ambaye ni mrithi wa mke wa Mafufu zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii hali iliyowafanya watu wengi kumpongeza kwa kumpata mrembo ambaye wanaendana naye kuanzia dini na sifa nyingine zote alizonazo.

“Umeona hiyo picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii? Huyo mrembo ambaye anatarajiwa kuolewa na Mafufu ambaye anasema Mungu ndiye kampa huyo kwani yule wa kwanza hakuwa chaguo la Mungu,” alisema Neema ambaye ni rafiki wa karibu na mrembo huyo.

Ili kupata ukweli kuhusu habari hizo, Amani lilimtafuta Mafufu ambaye alikiri kwamba ni kweli huyo mrembo ambaye anatambulika kwa jina la Upendo Meja ndiye anayetarajia kumuoa na atachukua nafasi ya aliyekuwa mkewe.

“Unajua nimekaa muda mrefu sana bila kuwa na mwanamke maana mke wangu aliondoka siku nyingi sana sema nilikuwa nafanya siri tu, hivyo kwa sasa naamini huyu Upendo ni Mungu ameniletea na natarajia kufunga naye ndoa hivi karibuni tu,” alisema Mafufu.

 

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Comments are closed.